Katavi Youth Mappers Chapter
Taarifa za awali
Barua pepe
katavimappers@gmail.comJina kamili la muombaji
Agness Kayegele
Una akaunti ya OSM?
Hapana
Ikiwa ndio taja jina lako la matumizi ya OSM kama hakuna andika N/A
Agness Kayegele
Tafadhali taja majina kamili na majina ya akaunti ya OSM ya mtu yeyote wa ziada atakayeongoza utekelezaji wa mradi ikiwa programu hii itafanikiwa
Apolinary Mushi, Songambele Otaru
Ikiwa una akaunti ya OSM Tafadhali tiki kwenye visanduku hali yako ya uchanguaji
Mgeni katika uchangiaji
Taja jina la kikundi cha jamii / shirika linawasilishwa kwa niaba ya katika maombi haya
KATAVI YOUTH MAPPERS CHAPTER
Je! Shirika lako / kikundi cha jamii kimesajiliwa kisheria?
Hapana
Ikiwa umeonyesha hapana hapo juu, tafadhali andika jina la shirika ambalo litaweza kupokea pesa za udhamini kwa niaba yako.
KATAVI NEW DEVELOPMENT VISION 2020
Taja Pendekezo la eneo la mradi utakapofanyika
MKOA WA KATAVI
Je! Hapo awali ulishapewa ufadhili wowote wa mradi?
MKOA WA KATAVI
Tafadhali onyesha jumla ya kiwango cha pesa unayoomba kwa TSH
9,150,000 Tshs
Taarifa Kuhusu Mradi
Je! Ni shida gani ambayo utafanyia kazia au kushughulikia ili kuitatua katika jamii yako?
(Katika sehemu hii tafadhali fafanua kwa kina changamoto ambayo mradi wako unashughulikia.Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Mkoa wa Katavi una changamoto na hasa katika idara ya afya na hasa kwa kupakana kwake na Nchi ya Congo na Burundi.Nchi hizi mbili pamoja na kuwa na changamoto za magonjwa ya milipuko kama ebola na kipindupindu na matatizo ya magonjwa mengine ya maambukizi ambayo huchangiwa na mwingiano mkubwa wa watu kama Ugonjwa wa UKIMWI na Kifua kikuu(TB) hasa kwenye machimbo ya dhahabu.Kwahyo lengo kuu la mradi huu ni kuweza kumapp vituo vyoe vya afya na hospitali na wagonjwa wote wa kifua kikuuu katika Mkoa wa Katavi.Kuna vituo vya Afya vya Serikali na binafsi 110 na Wagonjwa wa Kifua Kikuu wapo 700 na kati ya hao kuna baadhi amabo wa ugonjwa kifua kikuu sugu(CHRONIC TB-TB-DOT)
Ni nini kinachokuchochea kufanyia kazi suala hili?
(ni nini sababu iliyosababisha, imekuhimiza ufanye kazi juu ya suala hili, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Tukiweza kumapp hospitali na vituo vyote vya afya vya Mkoa itakuwa rahisi katika ufuatiliaji. utekelezaji wa mikakati na kupanga bajeti sahihi.Na kwa upande wa wagonjwa wa kifua kikuu na hasa wale SUGU.Tukijua idadi yake na takwimu zikapelekwa kwa wahusika.wadau kama kwa Ofisi ya Mganaga Mkuu wa Mkoa itakuwa ni rahisi kataika utekelezaji wake.Ugonjwa wa Kifua Kikuu na hasa kile kifua sugu ni hatari sana kwa jamii kama hakitadhibitiwa kwahiyo kujulikana na kubainishwa kwa wagonjwa hawa itakuwa ni hatua sahhi katika kudhibiti ugonjwa huu wa kifua kikuu.
Umewahi kufanya kazi kutatua shida hiyo hapo awali?
Hapana
Ikiwa ndio Umefanya nini tayari kutatua suala hili?
(Tafadhali eleza na onyesha mafanikio yako makubwa, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A
N/A
Ikiwa ndio Ni changamoto zipi ulizokabiliana nazo katika kazi yako ya kutatua suala hili, na ulitatua vipi changamoto hizo?
(Tafadhali bainisha na onyesha changamoto zako kubwa ulizokumbana nazo na ulizitatua vipi, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A
N/A
Ikiwa hapana, unatarajia changamoto gani wakati unafanya kazi ya kutatua suala hilo?
(Tafadhali bainisha na onyesha changamoto unazo his utakumbana nzo kaika utekerezaji wa mradi huu. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na
yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A
Changamoto kubwa itakuwa kufikia vituo na hospitali ambazo zipo maeneo ya mbali na hasa ziwani Tanganyika.Kuna maeneo ni magumu kufikikika. Na kwa upande wa wagonjwa wa kifua kikuu kuna wengine pia wapo katika vijiji vya ndani na vingine mahali pagumu kufikikika.na changamoto nyingine ni katika kufundisha watu jinsi ya kutumia open data source tools.Ni elimu na ujuzi mgeni kwahiyo itahitaji uvumilivu katika kufundisha mappers wapya.Na mwisho utayari wa kupewa ushirikiano na hasa kwa wagonjwa wa kifua kikuu na hasa kifua kikuu sugu.
Eleza ni upi mpango wako endelevu
(Katika sehemu hii tafadhali fafanua jinsi shughuli zako zitaendelea baada ya ufadhili. Ikiwa unaomba ufadhili wa kununua vifaa, eleza ni nani atakayehifadhi / kutumia vifaa unavyonunua, na kama una mipango endelevu wa maendeleo ya jamii yako. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
KATAVI YOUTH MAPPERS ni kikundi tumekianzisha kipya ambacho kinajumuisha wanafunzi wa chuo cha afya cha Katavi na vijana wengine Mkoani Katavi. Kwahiyo mpango wetu wa muda mrefu ni kuoona hii chapter inaendelea na kuwa na wajumbe wengi na elimu ya open data source tools inaendelea na kukua katika Mkoa.Mpango mwingine ni kuona jinsi gani hizi data tutakazokuwa tunazikusanya ziweze kutusaidia katika kutatua matatizo na kuweza kuboresha maisha ya watanzania
Lengo la Mradi
Je! Mradi huu una malengo gani katika jamii?
(Tafadhali elezea malengo ya mradi. Hii inaweza kujumuisha: kuweka malengo kama "tutafundisha idadi ya X ya jamii mpya," tutasajili kama taasisi ya kisheria ", au" data itatumiwa na X ", na kwanini malengo haya ni muhimu kwa jamii yako kama vile "tunakusudia kushirikisha idadi ya X ya wanawake katika shughuli za kuchora ramani ili tuweze kuwawezesha wanawake wa eneo hili" Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 150 na yasizidi maneno 300.)
1.Kusajiri hii KATAVI YOUTH MAPPERS kama Taasisi kisheria katika kufuata sheria zote za msajiri wa NGO Tanzania
2.Kueneza elimu ya open data source tools katika Mkoa wa Katavi na kuendelea kuchora ramani mbalimbali katika Mkoa wa Katavi
3.kukusanya idadi ya vituo vyote vya afya na hospitali za Serikali na Binafsi na kuziwasilisha kwa wadau wa afya wa Mkoa
4.Kudhibiti maambukizi na usambaaji wa ugonjwa wa kifua kikuu katika Mkoa wa Katavi. Wagonjwa wote wapatao 700 watabainishwa na kujulikana hali yao na jinsi gani ya kuweza kufuatilia maendeleo yao ya afya na udhibiti wa maambukizi mapya,Kupata data hizi ni muhimu mno Mkoani kwani ni rahisi kufuatilia pia sehemu yenye maambukizi makubwa treatnment trend na kufanya planning na budgeting.
Je! Malengo ya muda mrefu ya mradi ni yapi?
(Tafadhali eleza maono ya mradi wako. Hii inaweza kujumuisha: ambapo unaweza kuona mradi wako kwa muda wa miaka mitano, jinsi unataka data yako itumiwe, ushirikiano wa baadaye ambao ungetaka kuanzisha, au jinsi ungependa mradi wako ukue apo baadae Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300)
1 Kuweka kwenye ramani vituo vyote vya afya na hospitali kutasaidia katika zoezi zima la kuboresha huduma katika vituo husika kwani itakuwa kujua vipo wapi na vina mahitaji gani na rahisi kwa viongozi wa kuanzia Mkoani mpaka vijijini kujua hali ya vituo ,mapungufu na marekebisho
2.Kutasaidia kufuatilia ufuatiliaji na hasa wa magonjwa ya milipuko kwa kujua yanapotokea na jinsi yanavyoenea na hasa kwa kutumia hizi data huru(Open data source tools)
3.Kuakikisha elimu hii ya data huru inaenea kwa haraka na kupata na kuwafundisha wajumbe wengi na hasa wanachuo wa chuo cha afya cha Katavi na vijana wengine katika Mkoa wa Katavi
Orodhesha zana/vifaa unavyotarajia kutumia wakati wa mradi wako na kwanini
(Tafadhali eleza ni zana/vifaa zipi unapanga kutumia kukusanya, kusasisha, kusafisha, au kuhifadhi data na kwanini. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Open data kit(ODK) , Maps Me na Kobotool box tutaitumia kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu
Je! Unahitaji maarifa au ujuzi gani wa ziada ili kuboresha ufanisi wa mradi?
(ikiwa kuna mafunzo yoyote ya kuongeza utahitaji mfano jinsi ya kutumia zana za chanzo wazi, jinsi ya kuandika ripoti nzuri nk tafadhali elezea hapa chini na kwanini, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 nayasizidi maneno 300) Ikiwa hauna andika N/A
Sisi kama kikundi tungependa kuelimishwa zaidi katika jinsi ya kutumia kobo tool box na ARC Calculator
Eleza jinsi unavyopanga kusambaza ujumbe wako/mafanikio ya mradi kwa jamii
(Tafadhali toa mifano njia utatumia kuambaza ujumbe wako kwa wengine. Hii inaweza kujumuisha: jinsi utakavyotangaza habari yako, wapi utaonesha yaliyomo kwenye vyombo vya habari , jinsi utatumia njia za mitandao ya kijamii,. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Kwanza hizi data za vituo vya Afya na Hospitali kwenye Mkoa wa Katavi zinahitajika kwenye ofisi ya Mganga Mkuu waMkoa(RMO) Anazihitaji data hizi ili aweze kuziweka kwenye kandidata yake ya Mkoa kwa ajli ya kuangalia mapungufu na kurahisisha ufuatiliaji wake katika utendaji.Kuhusu hili la pili la Kuchua ramani na kumapp wagonjwa wote wa Kifua kikuu katika Mkoa wa Katavi kutaisaidia katika ufuatiliaji na kudhibiti ueneaji wa ugonjwa huu wa kifua kikuu.Mgonjwa wa kifua kikuu na hasa wale SUGU wasipobainishwa na kufuatiliwa kwa matibabu madhara yao ni makubwa sana.Kwa kitaalamu huwa wanajulikana kama TB-DOT hawa ni hatari sana kama wasipobainishwa na kufuatiliwa kwa matibabu na hasa uanzishwaji wa tiba na dawa.
Kwahiyo ujumbe utawakilishwa kwanza kwenye Ofisi ya Mganga Mkuu na wadau wengine wa maendeleo kwa utekelezaji
Umilikishwaji
Eleza ni nani atakayemiliki / kupata/kunufaika na kutumia data au mafunzo yatokanayo na mradi huu
(Ni muhimu kwamba data unayotengeneza wakati wa mradi iwe na matumizi , na kwamba itatumika kutatuta changamoto za kibinadamu au za kimaendeleo katika jamii. Katika sehemu hii, tafadhali jumuisha: ikiwa data utakayokusanya imeombwa na nani, ikiwa kuna uhusiano rasmi na shirika lolote, na ikiwa kuna MoU iliyopo kati yako na shirika unaloloshirikiana, na kwa muda gani umekuwa ukifanya kazi na shirika unaloshirikiana nalo. Ikiwa shirika lako au jamii itakuwa mtumiaji wa data, tafadhali fafanua jinsi watakavyotumia data hiyo, na watafikiaje/wataipataje data pia kuna uwezekano wa mashirika mengine yanayofanana kupata na kumiliki data hiyo?. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 400.)
Data hizi zimeombwa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi na zitatumika katika kuboresha utendaji wa kazi na huduma nyingine za afaya na jamii katika Mkoa wa Katavi.
Eleza kama kuna jamii / shirika lingine lolote unalopanga kulikaribia na kushirikiana ili kuwapatia data kwa madhumuni ya kukuza lengo la mradi
(Katika sehemu hii, tafadhali fafanua washirika wowote wa ziada ambao unaweza kuwakaribia au kushiriki data nao kwani wameonyesha hitaji la data itakayokusanywa. Ikiwa hakuna washirika wa ziada (zaidi ya mtumiaji wa data) hii lazima isemwe hapa. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) ikiwa
hakuna andika N / A
Tuna Mpango wa kuwapa hizi data shirika la Red cross Katavi na Chuo cha afya cha Mkoa wa Katavi kwani zitasaidia kataika utekelezaji wa shughuri mbalimbali zitakazokuwa na mahusiano na data tutakazokusanya
Ujumuishwaji
Utahakikishaje kuwa shughuli zako za mradi zitazingatia jinsia au watoto?
(Tafadhali eleza jinsi utakavyoshirikisha wanawake / wasichana au watoto wa shule katika shughuli zako za mradi. Tafadhali ingiza idadi ya wanawake, wasichana au vikundi vilivyotengwa unavyopanga kufanya nao kazi , na wakati gani katika shughuli zako unapanga kuwashirikisha. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300).
Mpaka muda huu idadi kubwa ya wajumbe katika kikundi chetu cha KATAVI YOUTH MAPPERS kina wajumbe wengi wa kike na katika mradi huu kama vituo hivi vyote tutakavyoviweka kwenye ramani vitasaidiwa na kufanyiwa maboresho wanufaika wakubwa kwenye hivi vituo ni watoto na wakina mama.Na magonjwa mengine ya mlipuko huwa yanathiri zaidi kin mama na watoto na hasa kwenye vituo vya afya avya mpakani na Nchi ya Congo waathirika wengi wanaosaidiwa kwenye vituo hivi ni kina mama na watoto.wengine wanakuja kama wakimbizi wakinwa aidha na vidonda, majeraha au magonjwa na sehemu pekee zitazosaidia kutoa huduma itakuwa ni hvi vituo na hospitali ambazo tutakuwa tumeziweka kwenye ramani.Na kuhusu wagonjwa wa kifua kikuu pia kama hawatabainishwa na kupatiwa matibabu watoto watakuwa kwenye hatari kupata maambukizi kwani kinga yao bado ni dhaifu
Mapinduzi ya ujuzi huria
Eleza jinsi unavyopanga kupanua jamii yako kwenye swala zima la matumizi/utengenezaji wa ramani/data
(Katika sehemu hii, tafadhali ainisha : njia yako utakayotumia kufanya kazi katika eneo la pembezoni mwa tanzania ili kupanua maarifa, utashirikishaje na jamii mpya kutoka kwa jamii isiyojulikana, idadi ipi ya watu wapya unaopanga kufanya nao kazi , na unampango gani ili uweze kudumu nao muda wote wa mradi na zaidi. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Kikundi chetu hiki kipya cha KATAVI YOUTH MAPPERS tuna mpango wa kueneza elimu hii ya kupanua maarifa ya open data source tools kwa vijana na hasa wanachuo cha afya cha Katavi na chuo cha maendeleo ya jamii cha msaginya-Mpanda katika Mkoa wa Katavi. Tuna mpango wa kufikia idadi ya members kuanzia 200 na kuendelea. Changamoto kubwa ya vijana wa Mikoa hii ya pembezoni kama Katavi ni ukosefu wa vitendea kazi kama kuwa na simu za smart phones. Tunaendelea kuwafundisha jinsi ya kutumia hizi open data tools hata kwa kutumia simu za marafiki na kwasababu tuna ofisi kubwa ambayo tunategemea kuweka computer ambayo itakuwa inatumiwa na members wa kativi youth mappers kwa kujifuzia na ukusanyaji wa data
Ushirikiano
Eleza jamii ambazo tayari unafanya kazi nazo
(Hii inaweza kujumuisha serikali za mitaa, sekta binafsi, taasisi au jamii za OSM (kama mifano). Ikiwa haujafanya kazi na jamii yoyote hapo juu, tafadhali sema hilo na ueleze jinsi unavyopanga kufanya kazi na jamii zingine katika mradi wako).Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Tunafanya kazi na Crowd 2 Map ya Janet Chapman na Good Hravest Organization ambao ndio walitutambulisha kwa Janet chapman wa crowds 2 map.
Eleza jamii zingine unazopanga kuwasiliana nazo, au kuanzisha uhusiano na, kwa madhumuni ya mradi huo
(Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Tunapenda kuanzisha mahusiano na Red cross katavi branch na Halmashauri zote katika Mkoa wa Katavi na Ofisi ya Takwimu ya Mkoa.Chuo cha VETA KATAVI nacho pia kipo katika malengo yetu ya kufanya nao kazi hapo baadaye
Viambatanishi
Tafadhali amabatanisha toleo la PDF la bajeti yako uliyopendekeza
(Bajeti yako lazima iwe ya kina na ya kweli. Mahesabu yanapaswa kuwa sahihi, na matumizi ya bajeti yanapaswa kuakisi na shughuli zilizoelezewa katika mpango wa mradi. Lazima utoe maelezo kwa nini unahitaji kitu unachotengenezea bajeti. Kwa kutumia mfano huu wa bajeti. https://docs.google.com/document/d/1sGPkshy6uZGlqtJHw1ipdplw9LmLUFvDF1B3RFAAU edit?usp=sharing. Hakikisha unaandika jina la mradi kama jina la PDF ukayotuma)
Tafadhali ambatanisha toleo la PDF la mpango wako wa mradi uliyopendekeza
(Mpango wa mradi lazima uwe wa kweli, na lazima utoe ratiba ya kina ya shughuli zilizoainishwa katika programu yako. Tunapendekeza kwamba ueleze shughuli zako kwa ufupi na uoanishe kwa wazishughuli hizo kwa kulingana na maelezo ya bajeti yako. Kwa kutumia mfano huu wa mpango kazi
https://docs.google.com/spreadsheets/d/1rLcERRARB2slRrgySPTmj_kWexV3d3IhPWSJsCBUlyg/edit?usp=sharing Hakikisha unaandika jina la mradi kama jina la PDF ukayotuma)
Uwasilishwaji
ikiwa inafaa, tafadhali weka link ya tovuti ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A
Bado hatujafungua website ila tuna mpango wa kufungua tovuti siku za karibuni
Ikiwezekana, tafadhali weka link ya akaunti ya facebook ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A
Tupo bado kwenye mchakato wa kufungua akaunti ya facebook
Ikiwezekana, tafadhali weka link ya akaunti ya twitter ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A
N/A
Je! ufadhili huu utafadhili mradi uliowekwa/unaofanyika tayari?
Hapana
Tafadhali thibitisha kuwa umekagua maombi yako, na umejibu maswali kwa kadiri ya uwezo wako
Ndio - ningependa kuwasilisha ombi langu