Lake Victoria Shore Environmental HIV/AIDS Project Tanzania (LAVISEHA)
Taarifa za awali
Barua pepe
laviseha2013@gmail.com
Jina kamili la muombaji
Paulo Lughali
Una akaunti ya OSM?
Ndio
Ikiwa ndio taja jina lako la matumizi ya OSM kama hakuna andika N/A
laviseha2013
Tafadhali taja majina kamili na majina ya akaunti ya OSM ya mtu yeyote wa ziada atakayeongoza utekelezaji wa mradi ikiwa programu hii itafanikiwa
Clement Ndaki (cndaki2005), Happiness Sylivester (hsylivester), Mecktrida Paulo (mpaulo84), Brighton Sylivester (brightsyliv), Nicklass Nyanda (Nicklas1997)
Ikiwa una akaunti ya OSM Tafadhali tiki kwenye visanduku hali yako ya uchanguaji
Mchangiaji wa mara kwa mara
Taja jina la kikundi cha jamii / shirika linawasilishwa kwa niaba ya katika maombi haya
Lake Victoria Shore Environmental HIV/AIDS Project Tanzania (LAVISEHA)
Je! Shirika lako / kikundi cha jamii kimesajiliwa kisheria?
Ndio
Ikiwa umeonyesha hapana hapo juu, tafadhali andika jina la shirika ambalo litaweza kupokea pesa za udhamini kwa niaba yako.
N/A
Taja Pendekezo la eneo la mradi utakapofanyika
Wilaya ya Magu magharibi (Mkoa wa Mwanza)
Je! Hapo awali ulishapewa ufadhili wowote wa mradi ?
Ndio
Tafadhali onyesha jumla ya kiwango cha pesa unayoomba kwa TSH
11,282,000
Taarifa Kuhusu Mradi
Je! Ni shida gani ambayo utafanyia kazi au kushughulikia ili kuitatua katika jamii yako?
(Katika sehemu hii tafadhali fafanua kwa kina changamoto ambayo mradi wako unashughulikia.Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Mradi wa kusaidia Kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Magu magharibi kwa mfumo ramani ya wazi ya OSM hususani kwa mbinu ya Maps.Me. Mradi huu unalenga kutatua changamoto za kijamii kwenye maeneo husika katika Wilaya ya Magu. Mradi utafanyika katika tarafa 1 miongoni
mwa tarafa 4 za Wilaya yote. Tarafa hiyo ni Sanjo ambayo ina jumla ya kata 7 na vijiji 22. Kwa kutumia mbinu ya ramani na ukusanyaji taarifa, mradi utachambua matatizo yanayohusiana na ukatili wa kijinsia katika jamii ambao unarudisha nyuma maendeleo katika jamii husika. Katika jamii nyingi za Tanzania, ikiwamo jamii ya watu wa Wilaya ya Magu, ukatili wa kijinsia wa aina mbalimbali kama vile ukeketaji kwa wasichana, ubakaji, mfumodume unaonyanyasa wanawake, kuozwa kwa lazima na kabla ya umri wa kuolewa, utumikishwaji kazini na kingono kwa watoto wa kike, rushwa ya ngono na kupigwa kwa wanawake vimetawala sana. Kupitia mradi huu wa ukusanyaji wa taarifa za ramani, elimu itatolewa ya kuzuia ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuchukua hatua kwa waathirika, mabingwa, viongozi wa Serikali na viongozi wa vikundi vya jamii. Sambamba na changamoto hii, wakati wa shughuli za ramani mradi pia utabaini katika Wilaya ya Magu magharibi changamoto zingine za kimaendeleo ambazo kwa sasa zipo kama vile ukosefu wa maji safi na salama, upungu wa kipato, barabara mbovu, ukosefu wa masoko ya bidhaa, ukosefu wa shule na vyuo, ukosefu wa nyumba bora, ukosefu wa zahanati, ukosefu wa majosho ya kuogesha mifugo, ukosefu wa mashine za kusaga na kukoboa, ukosefu wa nishati na upungufu wa rutuba ya ardhi. Katika changamoto hizi, mradi utaandaa ripoti itakayoisadia Serikali katika ngazi zote husuka kutambua maeneo yenye changamoto na kufanya maboresho kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.
Ni nini kinachokuchochea kufanyia kazi suala hili?
(ni nini sababu iliyosababisha, imekuhimiza ufanye kazi juu ya suala hili, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Tumeamua kufanya Mradi huu baada ya kutambua madhara yanayotokana na ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Magu. Kwa sababu ya ukatili wa kijinsia, watoto wengi hasa wa kike wamepata madhara ya kiakili, kiafya, kielimu, kimahusiano na kiuchumi. Wengine wao wameishia kujiingiza katika shughuli haramu kama vile kuondoka nyumbani na kwenda kuishi na kufanya kazi mtaani, kujiuza kimapenzi, kutumia madawa ya kulenvya na kutumikishwa kikazi. Lakini pia wengine wamekosa haki zao za msingi kama vile elimu, afya, makazi, malezi, kuepukana na kutengwa kwa sababu ya ulemavu/kasoro ya maumbile, uhuru wa kufanya kile wanachochagua na kuendeleza vipaji vyao. Wanawake pia kwa kutokujua wanachotakiwa kufanya wamedhulumika haki zao za kindoa ikwamo mirathi, mali, ushirikishwaji katika shughuli za kifamilia na kijamii. Pia wanawake wametendewa ukatili wa kimapenzi, kimwili na kiakili na kubaki wanaumia kwa sababu hawajui cha kufanya. Kwa hiyo mradi wetu kupitia shughuli za ramani na kukusanya taarifa mbalimbali kwa kushirikiana na waathirika utahamasisha na kuelimisha kuhusu kutambua ukatili wa kijinsia ni nini, madhara yake ni nini, jinsi ya kujikinga na jinsi ya kuchukua hatua kwa waathirika. Pia mradi wetu utatengeneza mpango endelevu wa kushughulikia tatizo la ukatili wa kijinsia kwa kuandaa na kushirikiana na mabingwa wa kushughulika na tatizo, serikali na sekta binafsi kupitia mradi huu, tutaainisha maeneo kwenye ramani ambayo ukatili umekithiri ili kusaidia jitihada za kutokomeza kabisa ukatili wa kijinsia. Pia tunatambua jitihada zilizopo za Serikali na sekta binafsi katika kuleta maendeleo katika Wilaya ya Magu. Hivyo, mradi utaunganisha jitihada za Serikali, sekta zingine binafsi na za mradi wetu ili kuleta maendeleo katika Wilaya ya Magu.
Umewahi kufanya kazi kutatua shida hiyo hapo awali?
Ndio
Ikiwa ndio Umefanya nini tayari kutatua suala hili?
(Tafadhali eleza na onyesha mafanikio yako makubwa, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A
Shirika letu limewahi kufanya kazi ya kushughulikia ukatili wa kijinsia katika Mkoa wa Mwanza. Katika mradi wetu wa siku za nyuma wa mwaka mmoja wa Kuunganisha Familia, tumeweza kutambua watoto (wasichana na wavulana) ambao wamefanyiwa ukatili wa kijinsia na kuamua kutoka nyumbani na kwenda kuishi na kufanya kazi katika jiji la Mwanza. Katika mradi huo, tuliwapata watoto mtaani jijini Mwanza katika kazi zetu za mtaani. Tuliongea nao na kutambua shida zao, tuliwashauri na kuwaunganisha na familia zao katika sehemu mbalimbali za mkoa wa Mwanza ikiwamo Wilaya ya Magu. Mojawapo ya sababu zilizowafanya kutoka nyumbani kwao ni ukatili wa kijinsia waliofanyiwa nyumbani kwao. Takribani watoto 23 (watoto wa kike 18, wa kiume 5) walisema wamewahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia na wazazi wao wa kufikia/kambo na watu wengine katika jamii/mtaa. Tuliwaunganisha na familia zao kwa kufanya ushauri nasaha/elimu kwa watoto na wazazi/walezi, kutoa elimu/mafunzo ya jinsi ya kuboresha maendeleo katika ngazi ya familia, kushirikisha Maafisa wa Ustawi wa Jamii Jiji, Wilaya na Kata, Dawati la polisi la Jinsia na Watoto, Viongozi wa Chama na Serikali katika ngazi ya Kata, Kijiji/Mtaa/Kitongoji, mashirika mengine, viongozi wa dini na waalimu wa shule za msingi na sekondari. Katika ngazi ya familia katika kuunganisha familia pia tumeweza kubaini kuwa wanawake wengi wametendewa ukatili wa kijinsia na waume wao/ndugu wa waume wao, wamedhulumiwa, wametelekezwa na wametengwa. Tuliweza kuwasaidia kwa kutoa elimu ya jinsi ya kuzuia ukatili wa kijinsia na kuchukua hatua tukishirikiana na Maafisa wa Ustawi wa Jamii Jiji, Wilaya na Kata, Dawati la polisi la Jinsia na Watoto, Viongozi wa Chama na Serikali katika ngazi ya Kata, Kijiji/Mtaa/Kitongoji, mashirika mengine, viongozi wa dini na waalimu wa shule za msingi na sekondari.
Ikiwa ndio Ni changamoto zipi ulizokabiliana nazo katika kazi yako ya kutatua suala hili, na ulitatua vipi changamoto hizo?
(Tafadhali bainisha na onyesha changamoto zako kubwa ulizokumbana nazo na ulizitatua vipi, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A
Shirika lilikumbana na changamoto katika mradi wetu wa siku za nyuma wa Kuunganisha Familia. Changamoto hizo tulizitatua kwa kushirikisha Maafisa wa Ustawi wa Jamii Jiji, Wilaya na Kata, Dawati la polisi la Jinsia na Watoto, Viongozi wa Chama na Serikali katika ngazi ya Kata, Kijiji/Mtaa/Kitongoji, mashirika mengine, viongozi wa dini na waalimu wa shule za msingi na sekondari. Changamoto hizo ni pamoja na:
a. Wazazi/walezi kukataa kuwapokea watoto katika hatua za awali kwa sababu ya ukatili waliofanyiwa. Changamoto hii tuliitatua kwa kutoa ushauri nasaha/elimu kwa watoto na wazazi/walezi.
b. Tabia za utukutu ambazo watoto wameiga kutoka mtaani. Changamoto hii tuliitatua kwa kufanya mazoezi ya uponyaji kisaikolojia na kiafya kwa kutumia mbinu za ushauri, kutambua vipaji vyao na kuviendeleza kwa kuwashirikisha wazazi/walezi na waalimu wa shule, yoga, dini, michezo, kuwarejesha shuleni na kutoa elimu/mafunzo ya jinsi ya kuboresha maendeleo katika ngazi ya familia.
c. Umaskini uliokithiri. Baadhi ya familia zilikuwa na umaskini wa kiwango cha juu. Changamoto hii tuliitatua kwa kutoa elimu/mafunzo ya jinsi ya kuboresha maendeleo katika ngazi ya familia.
d. Kutengana kwa wazazi. Wazazi wa baadhi ya watoto walikuwa wametengana. Changamoto hii tuliitatua kwa kutafuta mzazi/ndugu aliye tayari kumpokea mtoto na kutoa ushauri.
e. Ukosefu wa ukweli na uwazi kwa waliofanyiwa ukatili wa kijinsia. Kitendo cha kufanyiwa ukatili wa kijinsia ni jambo la aibu kwa yule aliyetendewa. Hivyo, baadhi ya waathirika walikataa kusema ukweli na uwazi. Changamoto hii tuliitatua kwa kutoa ushauri ili kutengeneza mazingira ya wao kutuamini sisi na kuwa na uhusiano mzuri na wao ili waweze kutoa taarifa kamili.
Ikiwa hapana, unatarajia changamoto gani wakati unafanya kazi ya kutatua suala hilo?
(Tafadhali bainisha na onyesha changamoto unazo his utakumbana nzo kaika utekerezaji wa mradi huu. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na
yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A
N/A
Eleza ni upi mpango wako endelevu
(Katika sehemu hii tafadhali fafanua jinsi shughuli zako zitaendelea baada ya ufadhili. Ikiwa unaomba ufadhili wa kununua vifaa, eleza ni nani atakayehifadhi / kutumia vifaa unavyonunua, na kama una mipango endelevu wa maendeleo ya jamii yako.Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Mradi huu utakuwa endelevu. Tumeweka mpango endelevu ambao utaendelezwa baada ya ufadhili. Tumepanga kutoa mafunzo ya jinsi ya kukusanya taarifa kupitia programu ya Maps.Me ambazo zitasaidia katika shuhuli za kupambana na ukatili wa kijinsia na kutambua ni wapi waathirika walipo na tutawafikiaje kiurahisi. Mafunzo haya yatafanyika kwa watu 80 ambao watakuwa ni viongozi wa vijiji, viongozi wa vikundi vya jamii na mabingwa (Viongozi 39 wa vijiji, viongozi 20 wa vikundi na mabingwa 21). Mafunzo yatafanyika wakati tunafanya shughuli zetu za ramani na pia kwa kuwakusanya sehemu moja ili kutoa mafunzo zaidi. Mafunzo yatawajengea uwezo wa kuendeleza shughuli za mradi baada ya ufadhili. Watakuwa na uwezo wa kuwafundisha watu wengine walioko katika vijiji au vikundi vyao na katika maeneo mengine bila uwepo wa ufadhili. Baadhi ya mabingwa watakuwa ni watu ambao wamewahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia ambao watakuwa na uchungu wa kujitolea kupambana na tatizo baada ya ufadhili. Kwa kuwa watafundishwa kuwa shughuli hizi zitakuwa ni kwa faida yao na jamii kwa ujumla, watatakiwa kujitolea kutumia simu zao katika kuendeleza shughuli za mradi baada uya ufadhili.Baada ya ufadhili, shirika la LAVISEHA litaendelea kushirikiana na wanufaika 80, serikali na sekta binafsi ili kufanya mradi kuwa endelevu. Na kwa kuwa shirika letu ninajihusisha na masuala VVU na UKIMWI, tutakusanya pia taarifa mbalimbali za maeneo hatarishi yanayopelekea ogezeko na maambukizi kama vile Bars na maeneo mengine ya starehe ili kujikita zaidi katika utoaji elimu kwenye maeneo hatarishi zaidi.
Lengo la Mradi
Je! Mradi huu una malengo gani katika jamii?
(Tafadhali elezea malengo ya mradi. Hii inaweza kujumuisha: kuweka malengo kama 'tutafundisha idadi ya X ya jamii mpya' tutasajili kama taasisi ya kisheria' data itatumiwa na X' na kwanini malengo haya ni muhimu kwa jamii yako kama vile tunakusudia kushirikisha idadi ya X ya wanawake katika shughuli za kuchora ramani ili tuweze kuwawezesha wanawake wa eneo hili' Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 150 na yasizidi maneno 300.)
Lengo Na. 1. Kufanya shughuli za ramani ili kukusanya taarifa - Shughuli zake ni kama ifuatavyo:
• Ukusanyaji wa taarifa za huduma za kijamii zilizopo kwenye kata husika.
• Kupunguza ukatili katika jamii kwa kupitia ukusanyaji wa taarifa na kutambua maeneo gani waathirika wanatokea zaidi.
• Kufanya kazi na waathirika 21 wa ukatili pamoja na dawati la jinsia ili kusaidia juhudi za upambanaji na tatizo la ukatili.
• Kufanya mafunzo kwa viongozi wa serikali na vikundi vya jamii na mabingwa ya ukusanyaji wa taarifa na kuziweka kwenye OSM.
• Mappers wa LAVISEHA tutapata mafunzo ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa na kuziweka kwenye OSM. (Tutaomba msaada wa mafunzo mengine kutoka OMDTZ).
• Kufanya vikao ofisini kuhusu mradi kila mwezi.
Lengo Na. 2. Kuhamasisha jamii na kutoa elimu juu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.- Shughuli zake ni kama ifuatavyo:
• Kufanya mafunzo kwa wanufaika 80 ya kuzuia ukatili wa kijinsia.
• Kutembelea viongozi wa serikali na wadau ili kufikisha ujumbe na kutambua waathirika mahali walipo.
• Kuongeza ujuzi wa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa Mappers 6 wa LAVISEHA.
• Kuunda timu ya mabingwa 21 ambao ni waathirika wa ukatili wa kijinsia na viongozi wengine 59.
Je! Malengo ya muda mrefu ya mradi ni yapi?
(Tafadhali eleza maono ya mradi wako. Hii inaweza kujumuisha: ambapo unaweza kuona mradi wako kwa muda wa miaka mitano, jinsi unataka data yako itumiwe, ushirikiano wa
baadaye ambao ungetaka kuanzisha, au jinsi ungependa mradi wako ukue apo baadae Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno
300)
Maono ya mradi ni kuwa na jamii isiyotendea wanawake na watoto ukatili wa kijinsia na inayohusisha wanawake katika shughuli za maendeleo. Lengo kuu la mradi ni kuunganisha jitihada za Serikali, sekta binafsi, jamii na mradi ili kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuleta maendeleo kwa kutumia na ukusanya taarifa za mfumo wa wazi wa OSM. Mradi utatengeneza mfumo endelevu katika eneo husika ili utumiwe na jamii katika kutokomeza ukatili wa kijinsia. Mradi kwa kutumia mafunzo utaandaa mabingwa wanawake 21, viongozi 39 wa vijiji na viongozi 20 wa vikundi vya wanawake vya maendeleo ambao kwa ujumla watakuwa na jukumu la kuendeleza shughuli za mradi katika maeneo yao na maeneo mengine ya wilaya nzima ya Magu katika miaka mitano ijayo kwa kushirikiana na shirika la LAVISEHA. Hivyo mradi utahakikisha kuwa jamii imeweka utaratibu wa pamoja wa kuondoa ukatili wa kijinsia na kuleta maendeleo ndani ya miaka mitano. Kwa kutumia shughuli za ramani za mfumo wa wazi wa OSM, mradi pia utaandaa taarifa ambazo zitatumiwa na shirika la LAVISEHA, jamii, serikali ngazi ya kata, kijiji, kitongoji, polisi (dawati la jinsia na watoto), ustawi wa jamii na sekta binafsi katika kuleta maendeleo na kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Orodhesha zana/vifaa unavyotarajia kutumia wakati wa mradi wako na kwanini
(Tafadhali eleza ni zana/vifaa zipi unapanga kutumia kukusanya, kusasisha, kusafisha, au kuhifadhi data na kwanini. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Mradi utatumia zana mbalimbali ili kukusanya, kusasisha, kusafisha, au kuhifadhi data. Zana hizo ni kama ifuatavyo:
a. Kadi kwa vikundi vya jamii. Mradi utatengeneza kadi maalumu zenye maswali yahusuyo mradi na kuzigawa kwenye vikundi vya jamii ambao watajaza kadi hizo. Hii itasaidia kupata data za kimaendeleo katika jamii na data za ukatili wa kijinsia katika jamii na pia kutambua waathirika wa ukatili wa kijinsia katika jamii.
b. “Questionnaires” za usahili wa ana kwa ana. Mradi utatengeneza “Questionnaires” kwa ajili ya usahili wa ana kwa ana utakaofanywa na mappers wa mradi na wanufaika 80 wakati wa shughuli za ramani kwa kutumia mfumo wa wazi wa Maps.Me. Hii itasaidia kuuliza maswali na kukusanya taarifa za kimaendeleo na ukatili wa kijinsia katika vijiji husika. Maswali yataulizwa kwa viongozi wa familia, vijiji. Shule, madhehebu, vikundi vya jamii, na watu wengine katika makundi mbalimbali ya jamii.
c. Mfumo wa Maps.Me kwa kutumia simu. Tutachukua moja kwa moja vitu vya maendeleo kwa njia ya simu kwa mfumo wa Maps.Me katika shughuli zetu za ramani. Hii itasaidiakuona kwa uhalisia maendeleo ya vijiji. Ramani itakayopatikana itaonyesha huduma mbalimbali pamoja na barabara ili kusaidia polisi, viongozi wa serikali ngazi ya kata na kijiji na wadau kufika kwa urahisi katika maeneo ambako ukatili wa kijinsia umefanyika. Pia ramani itasaidia shirika la LAVISEHA, serikali na wadau wa maendeleo katika kupanga na kufanya maendeleo.
d. Kumbukumbu za serikali ya kijiji/kata na sekta binafsi. Mradi utachukua kumbukumbu za serikali katika ngazi ya kijiji na kata zinazohusu ukatili wa kijinsia na maendeleo ili kuunganisha na data zilizopatikana kwa zana zingine. Hii itasaidia kupata data za jumla ambazo zitawasaidia viongozi wa serikali na wadau wa maendeleo katika kupanga na kufanya maendeleo.
Je! Unahitaji maarifa au ujuzi gani wa ziada ili kuboresha ufanisi wa mradi?
(ikiwa kuna mafunzo yoyote ya kuongeza utahitaji mfano jinsi ya kutumia zana za chanzo wazi, jinsi ya kuandika ripoti nzuri nk tafadhali elezea hapa chini na kwanini, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 nayasizidi maneno 300) Ikiwa hauna andika N/A
Katika mradi wetu tutahitaji mafunzo ya nyongeza ya jinsi ya kufanya shughuli za ramani za mfumo wa wazi wa OSM. Mafunzo haya yatafanywa kwa mappers 6 na mtaalamu wa GIS kutoka OMDTZ ambaye atatufundisha vitu vingi vinavyohusu shughuli za ramani kwa mfumo wa wazi wa OSM. Tutahitaji kupata mafunzo hayo ya nyongeza ili kuboresha ufanisi wa shughuli zetu za ramani na hivyo kuondoa makosa madogomadogo katika shughuli yote ya mradi. Hii pia itatusaidia sisi mappers kuwafundisha wanufaika 80 kwa ujuzi zaidi wakati wa shughuli zetu za ramani. Pia tutahitaji mafunzo ya nyongeza juu ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo haya yatafanywa kwa mappers 6 na Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Jiji la Mwanza. Hii itatusadia sisi mappers kuongeza ujuzi na maarifa katika suala zima la ukatili wa kijinsia na itatusaidia kufanya kazi kwa makini wakati wote katika mradi wetu wa kutokomeza ukatili wa kijinsia. Hii pia itatusaidia sisi mappers kuwafundisha wanufaika 80 kwa ujuzi zaidi juu ya ukatili wa kijinsia wakati wa shughuli zetu za ramani.
Eleza jinsi unavyopanga kusambaza ujumbe wako/mafanikio ya mradi kwa jamii
(Tafadhali toa mifano njia utatumia kuambaza ujumbe wako kwa wengine. Hii inaweza kujumuisha: jinsi utakavyotangaza habari yako, wapi utaonesha yaliyomo kwenye vyombo vya habari , jinsi utatumia njia za mitandao ya kijamii,. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Tutasambaza ujumbe kwa wengine kwa kutumia njia za mitandao ya kijamii. Tutatumia Whatsapp ambapo tutatengeneza kikundi cha WhatsApp ili kusambaza ujumbe kwa wengine. Pia mahojiano maalumu na wanajamii na viongozi wa vijiji yatarekodiwa kwa njia ya video na kusambazwa katika mtandao wa kijamii wa youtube. Matukio mbalimbali ya shughuli zetu ya mafunzo, uelimishaji jamii, ukusanyaji data na uhamasishaji katika jamii yatawekwa katika ukurasa wa facebook ili kusambaza ujumbe kwa wengine.(link ya ukurasa wa facebook: https://www.facebook.com/paulo.lughali.3).
Umilikishwaji
Eleza ni nani atakayemiliki / kupata/kunufaika na kutumia data au mafunzo yatokanayo na mradi huu
(Ni muhimu kwamba data unayotengeneza wakati wa mradi iwe na matumizi , na kwamba itatumika kutatuta changamoto za kibinadamu au za kimaendeleo katika jamii. Katika sehemu hii, tafadhali jumuisha: ikiwa data utakayokusanya imeombwa na nani, ikiwa kuna uhusiano rasmi na shirika lolote, na ikiwa kuna MoU iliyopo kati yako na shirika unaloloshirikiana, na kwa muda gani umekuwa ukifanya kazi na shirika unaloshirikiana nalo. Ikiwa shirika lako au jamii itakuwa mtumiaji wa data, tafadhali fafanua jinsi watakavyotumia data hiyo, na watafikiaje/wataipataje data pia kuna uwezekano wa mashirika mengine yanayofanana kupata na kumiliki data hiyo?. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 400.)
Mradi utatengeneza mfumo endelevu katika eneo husika ili utumiwe na jamii katika kutokomeza ukatili wa kijinsia. Mradi kwa kutumia mafunzo utaandaa mabingwa wanawake 21, viongozi 39 wa vijiji na viongozi 20 wa vikundi vya wanawake vya maendeleo ambao kwa ujumla watakuwa na jukumu la kuendeleza shughuli za mradi katika maeneo yao na maeneo mengine ya wilaya nzima ya Magu. Hivyo mradi utahakikisha kuwa jamii imeweka utaratibu wa pamoja wa kuondoa ukatili wa kijinsia na kuleta maendeleo. Kwa kutumia shughuli za ramani za mfumo wa wazi wa Maps.Me, mradi pia utaandaa taarifa ambazo zitaendelea kutumiwa na shirika la LAVISEHA, jamii, serikali ngazi ya kata/kijiji, polisi, Ustawi wa jamii na sekta binafsi katika kuleta maendeleo na kutokomeza ukatili wa kijinsia hata baada ya ufadhili. Pia mradi utaonyesha barabara zote katika eneo la mradi ili kuwawezesha polisi na viongozi wengine kuwafikia waathirika wa ukatili wa kijinsia kwa urahisi. Katika mkoa wa Mwanza ikiwamo wilaya ya Magu, shirika letu la LAVISEHA tangu 2015 limefanya kazi na shule za msingi na sekondari na vikundi vya maendeleo vya wanawake katika shughuli zake. Baadhi ya vikundi vya maendeleo vya wanawake katika eneo la mradi ambavyo LAVISEHA limefanya navyo kazi ni pamoja na Wajane Bujora, SAWAVU Kisesa, Masalikula Welamasonga, Kilimobiashara Igekemaja, Kazamoyo Nyanguge, Jirani umekuwaje Nyanguge, Muungano Bujora, Faraja Nyanguge, Kujitegemea Kitumba, Kwa Neema Isangijo, Umoja Ihayabuyaga, Agape Nyanguge, Upendo Bujora na Ushirikiano Mwamanga. Vikundi hivi vyote wako tayari kufanya kazi na mradi wetu na kutumia taarifa za mradi katika shughuli zao za maendeleo wakishirikiana na shirika la LAVISEHA. Katika shughuli zetu za ramani tumefanya kazi na Kata za Mhandu na Mahina katika Jiji la Mwanza. Pia katika wilaya ya Magu katika shughuli za ramani tunaendelea kufanya kazi na Kata za Bujora na Kisesa katika vijiji vya Kanyama, Bukerebe na Iseni Mlimani.
Eleza kama kuna jamii / shirika lingine lolote unalopanga kulikaribia na kushirikiana ili kuwapatia data kwa madhumuni ya kukuza lengo la mradi
(Katika sehemu hii, tafadhali fafanua washirika wowote wa ziada ambao unaweza kuwakaribia au kushiriki data nao kwani wameonyesha hitaji la data itakayokusanywa. Ikiwa hakuna washirika wa ziada (zaidi ya mtumiaji wa data) hii lazima isemwe hapa. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) ikiwa hakuna andika N / A
Baadhi ya vikundi vya maendeleo vya wanawake katika eneo la mradi ambavyo LAVISEHA limefanya navyo kazi ni pamoja na Wajane Bujora, SAWAVU Kisesa, Masalikula Welamasonga, Kilimobiashara Igekemaja, Kazamoyo Nyanguge, Jirani umekuwaje Nyanguge, Muungano Bujora, Faraja Nyanguge, Kujitegemea Kitumba, Kwa Neema Isangijo, Umoja Ihayabuyaga, Agape Nyanguge, Upendo Bujora na Ushirikiano Mwamanga. Vikundi hivi vyote wako tayari kufanya kazi na mradi wetu na kutumia taarifa za mradi katika shughuli zao za maendeleo. Katika wilaya ya Magu katika eneo la mradi serikali ngazi ya kata/kijiji, polisi, Ustawi wa jamii na sekta binafsi watatumia taarifa za mradi katika kuleta maendeleo na kutokomeza ukatili wa kijinsia hata baada ya ufadhili.
Ujumuishwaji
Utahakikishaje kuwa shughuli zako za mradi zitazingatia jinsia au watoto?
(Tafadhali eleza jinsi utakavyoshirikisha wanawake / wasichana au watoto wa shule katika shughuli zako za mradi. Tafadhali ingiza idadi ya wanawake, wasichana au vikundi vilivyotengwa unavyopanga kufanya nao kazi , na wakati gani katika shughuli zako unapanga kuwashirikisha. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300).
Mradi utafanya kazi na wanufaika 80 ambao kati yao wanawake ni 60 na wanaume 20. Katika yao hao, mabingwa watakuwa 21, viongozi 39 wa vijiji na viongozi 20 wa vikundi vya jamii vya maendeleo ambao kwa ujumla watakuwa na jukumu la kuendeleza shughuli za mradi katika maeneo yao na maeneo mengine ya wilaya nzima ya Magu katika miaka mitano ijayo kwa kushirikiana na shirika la LAVISEHA. Katika shughuli zetu za ramani tutatambua waathirika wa ukatili wa kijinsia ambao wengi wao ni wanawake na wasichana. Hivyo mafunzo ya shughuli za ramani kwa mfumo wa OSM kwa jamii na mafunzo ya kuzuia ukatili wa kijinsia yatahusisha kwa kiasi kikubwa wanawake na wasichana. Katika shughuli zetu za ramani kwa kutumia mfumo wa wazi wa OSM tutahoji na kutoa ushauri kwa wanawake na watoto (wasichana) wengi kwa kuwa mradi unawalenga wao kwa kiasi kikubwa.
Mapinduzi ya Ujuzi Huria
Eleza jinsi unavyopanga kupanua jamii yako kwenye swala zima la matumizi/utengenezaji wa ramani/data
(Katika sehemu hii, tafadhali ainisha : njia yako utakayotumia kufanya kazi katika eneo la pembezoni mwa tanzania ili kupanua maarifa, utashirikishaje na jamii mpya kutoka kwa jamii isiyojulikana, idadi ipi ya watu wapya unaopanga kufanya nao kazi , na unampango gani ili uweze kudumu nao muda wote wa mradi na zaidi. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Mradi wa Kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Magu magharibi kwa mbinu ya mfumo wazi wa OSM mradi unalenga kutatua changamoto za kijamii kwenye maeneo husika katika Wilaya ya Magu. Mradi utafanyika katika tarafa 1 miongoni mwa tarafa 4 za Wilaya yote. Tarafa hiyo ni Sanjo ambayo ina jumla ya kata 7 na vijiji 22. Eneo kubwa la mradi ni katika vijiji wilayani Magu. Mradi utafanya kazi na wanufaika 80 ambao kati yao wanawake ni 60 na wanaume 20. Katika yao hao, mabingwa watakuwa 21, viongozi 39 wa vijiji na viongozi 20 wa vikundi vya wanawake vya maendeleo ambao kwa ujumla watakuwa na jukumu la kuendeleza shughuli za mradi na ukusanyaji wa taarifa katika maeneo yao na maeneo mengine ya wilaya nzima ya Magu katika miaka mitano ijayo kwa kushirikiana na shirika la LAVISEHA.
Ushirikiano
Eleza jamii ambazo tayari unafanya kazi nazo
(Hii inaweza kujumuisha serikali za mitaa, sekta binafsi, taasisi au jamii za OSM (kama mifano). Ikiwa haujafanya kazi na jamii yoyote hapo juu, tafadhali sema hilo na ueleze jinsi unavyopanga kufanya kazi na jamii zingine katika mradi wako).Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Shirika linafanya kazi na viongozi wa serikali ngazi ya kata, kijiji, kitongoji, polisi (dawati la jinsia na watoto), shule za msingi na sekondari, ustawi wa jamii na sekta binafsi. Pia shirika linafanya kazi na vikundi vya maendeleo vya jamii ambavyo ni Wajane Bujora, SAWAVU Kisesa, Masalikula Welamasonga, Kilimobiashara Igekemaja, Kazamoyo Nyanguge, Jirani umekuwaje Nyanguge, Muungano Bujora, Faraja Nyanguge, Kujitegemea Kitumba, Kwa Neema Isangijo, Umoja Ihayabuyaga, Agape Nyanguge, Upendo Bujora na Ushirikiano Mwamanga. Vikundi hivi vyote wako tayari kufanya kazi na mradi wetu na kutumia taarifa za mradi katika shughuli zao za maendeleo wakishirikiana na shirika la LAVISEHA. Katika shughuli zetu za ramani tumefanya kazi na Kata za Mhandu na Mahina katika Jiji la Mwanza. Pia katika wilaya ya Magu katika shughuli za ramani tunaendelea kufanya kazi na Kata za Bujora na Kisesa katika vijiji vya Kanyama, Bukerebe na Mlimani. Tunategemea kupanua shughuli zetu za ramani katika mradi baada ya kupata ufadhili.
Eleza jamii zingine unazopanga kuwasiliana nazo, au kuanzisha uhusiano na, kwa madhumuni ya mradi huo
(Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)
Katika shughuli zetu za ramani kwa mfumo wa OSM na mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia, tunategemea kuwasiliana na jamii katika vijiji vingi katika wilaya ya Magu. Katika vijiji hivyo tutajenga uhusiano na serikali za vijiji. Pia tutajenga uhusiano na sekta binafsi na taasisi katika vijiji hivyo. Vijiji ambavyo tunategemea kuanzisha uhusiano navyo ni pamoja na Bugumangala, Matela, Muda, Nyanguge, Ijinga, Bundilya, Shinembo, Bugabu, Nyamahanga, Kahangara, Lugeye, Kitongosima, Kigangama, Kisesa B, Malilika, Misambo na Mwamanga.Tutajenga uhusiano na viongozi wa serikali za vijiji, vitongoji, kata, polisi (dawati la jinsia na watoto), ustawi wa jamii,
madhehebu, vikundi vya maendeleo vya jamii, shule na taasisi zingine na kuwapa elimu ya jinsi ramani na mfumo mzima wa OSM kupitia Maps.me unavyoweza kusaidia katika harakati mbalimbali za kijamii.
Viambatanishi
Tafadhali amabatanisha toleo la PDF la bajeti yako uliyopendekeza
(Bajeti yako lazima iwe ya kina na ya kweli. Mahesabu yanapaswa kuwa sahihi, na matumizi ya bajeti yanapaswa kuakisi na shughuli zilizoelezewa katika mpango wa mradi. Lazima utoe maelezo kwa nini unahitaji kitu unachotengenezea bajeti. Kwa kutumia hii templeti ya bajeti. https://docs.google.com/document/d/1sGPkshy6uZGlqtJHw1ipdplw9LmLUFvDF1B3RFAAU edit?usp=sharing. Hakikisha unaandika jina la mradi kama jina la PDF ukayotuma)
Tafadhali ambatanisha toleo la PDF la mpango wako wa mradi uliyopendekeza
(Mpango wa mradi lazima uwe wa kweli, na lazima utoe ratiba ya kina ya shughuli zilizoainishwa katika programu yako. Tunapendekeza kwamba ueleze shughuli zako kwa ufupi na uoanishe kwa wazishughuli hizo kwa kulingana na maelezo ya bajeti yako. Kwa kutumia templeti ya mpango kazi
https://docs.google.com/spreadsheets/d/1rLcERRARB2slRrgySPTmj_kWexV3d3IhPWSJsCBUlyg/edit ? usp=sharing. Hakikisha unaandika jina la mradi kama jina la PDF ukayotuma)
Uwasilishwaji
ikiwa inafaa, tafadhali weka link ya tovuti ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A
N/A
Ikiwezekana, tafadhali weka link ya akaunti ya facebook ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A
https://www.facebook.com/paulo.lughali.3
Ikiwezekana, tafadhali weka link ya akaunti ya twitter ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A
N/A
Je! ufadhili huu utafadhili mradi uliowekwa/unaofanyika tayari?
Ndio
Tafadhali thibitisha kuwa umekagua maombi yako, na umejibu maswali kwa kadiri ya uwezo wako
Ndio - ningependa kuwasilisha ombi langu